HABARI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshuhudia kusainiwa kwa hati mbalimbali za makubaliano baina ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


ikiwemo Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar(ZIPA) na Commonwealth Enterprise and Investment Council (CWEIC), Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia.

Zanzibar(ZPRA) na Taasisi ya Geopatners Ltd ya Uingereza, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Nutri-San Limited(UK) , the Scottish Association for Marine Science(UK) pamoja na Chuo cha Kilimo cha Royal(UK) katika ukumbi wa Guildhall Art Gallery, Jijini London tarehe 9 Aprili 2025. 
 Hati hizo za makubaliano zilizosainiwa zitaisaidia kuleta ufanisi zaidi sekta mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Buluu na Uwekezaji.

RAIS MWINYI AWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA WA UINGEREZA KUWEKEZA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo sekta ya Uchumi wa buluu, utalii, usafiri wa baharini, uvuvi , nishati na miundombinu ya kidijitali.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za biashara na uchumi za Uingereza kilichoandaliwa na Taasisi ya Eastern Africa Association ya Uingereza katika Jiji la London, tarehe 7 Aprili 2025.


Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema katika kipindi cha Miaka 4 Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua zaidi ya asilimia 7 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta mbalimbali.

Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa wawekezaji hao kuwekeza katika zao la Mwani, ameeleza kuwa Zanzibar ndio mzalishaji namba moja wa zao hilo Afrika ambalo soko lake linaendelea kukua zaidi.


MY MEDIA DIGITAL

Karibu My Media Digital! Hii ni blog inayohusu ubunifu wa kidigitali, ikihusisha video editing, graphic design, na content creation. Tunakuletea mbinu bora na maarifa ya kusaidia kuboresha kazi zako za digital media. Endelea kufuatilia kwa mafunzo, makala, na updates za kisanaa!

Post a Comment

Previous Post Next Post