MUIGIZAJI CARINA AFARIKI DUNIA AKIWA INDIA

 


MUIGIZAJI CARINA AFARIKI DUNIA AKIWA NCHINI INDIA

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Hawa maarufu kama Carina, afariki dunia akiwa nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kuhuzunisha zimeibuka leo Aprili 15, 2025, zikithibitisha kifo cha muigizaji mashuhuri wa filamu za Bongo, Hawa anayefahamika zaidi kwa jina lake la kisanii, Carina. Marehemu Carina alikuwa nchini India kwa ajili ya matibabu ya tatizo sugu la tumbo ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na familia, Carina alitarajiwa kurejea nchini Tanzania leo Aprili 15, baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa uliolenga kutatua tatizo hilo la kiafya. Hata hivyo, kabla ya kurejea, hali yake ilibadilika ghafla akiwa hospitalini na juhudi za madaktari kuokoa maisha yake hazikuzaa matunda.

Carina amekuwa miongoni mwa waigizaji waliogusa nyoyo za watu wengi kupitia kazi zake za sanaa, ambapo alivuma sana kupitia maigizo yenye maudhui ya kijamii na maisha halisi. Wapenzi wa filamu nchini na mashabiki wake wamepokea taarifa hizi kwa majonzi makubwa.

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kurejea nyumbani kwa ajili ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia kwa kushirikiana na serikali kupitia ubalozi wa Tanzania nchini India.


My Media Digital inaungana na familia, ndugu, jamaa, wasanii wenzake na mashabiki wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.



MY MEDIA DIGITAL

Karibu My Media Digital! Hii ni blog inayohusu ubunifu wa kidigitali, ikihusisha video editing, graphic design, na content creation. Tunakuletea mbinu bora na maarifa ya kusaidia kuboresha kazi zako za digital media. Endelea kufuatilia kwa mafunzo, makala, na updates za kisanaa!

Post a Comment

Previous Post Next Post