Rais Mwinyi: Zanzibar Yaendelea Kung'ara Kiuchumi, Ukuaji Wafikia Zaidi ya Asilimia 7

RAIS MWINYI:UCHUMI WA ZANZIBAR UMEKUA KWA ASILIMIA ZAIDI YA 7.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema katika kipindi cha Miaka 4 Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua kwa kasi zaidi ya asilimia 7 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta mbalimbali.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na Viongozi mbalimbali wa Wafanyabiashara wa Uingereza kilichoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika ukumbi wa Serikali ya Uingereza Jijini la London, tarehe 8 Aprili 2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo sekta ya Uchumi wa buluu, utalii, usafiri wa baharini, uvuvi , nishati na miundombinu ya kidijitali.
Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Uingereza wamehudhuria hafla hiyo akiwemo Alderman Professor Emma Edhen , Alderman City of London na Lord Malhard, House of Lords , na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Commonwealth, Lord Darroch wa House of Lords.


MY MEDIA DIGITAL

Karibu My Media Digital! Hii ni blog inayohusu ubunifu wa kidigitali, ikihusisha video editing, graphic design, na content creation. Tunakuletea mbinu bora na maarifa ya kusaidia kuboresha kazi zako za digital media. Endelea kufuatilia kwa mafunzo, makala, na updates za kisanaa!

Post a Comment

Previous Post Next Post