TAARIFA RASMI YA PONGEZI
Kwa Klabu ya Simba SC – CAF Confederation Cup
Na: [My Media Digital arena - TEAM WORK ], Mwakilishi wa Michezo – / MY MEDIA DIGITAL
Hongera nyingi kwa Klabu ya Simba kwa ushindi mkubwa katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi huu si tu kwamba umeleta furaha kwa mashabiki wenu, bali pia mmeipa heshima Tanzania nzima kwa kuipeperusha vyema bendera ya Taifa letu katika anga za kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kupitia taarifa iliyotumwa kwenye WhatsApp channel yake rasmi, leo saa 6:07 Jioni baada ya kumalizika kwa mchezo SIMBA VS STELLEN BOSCH, amewapongeza wachezaji, KWA ushindi na kuipa heshima nchi.
Kwa niaba ya wadau wa michezo nchini, tunawatia moyo Simba SC kuendelea na morali hiyo hadi kilele cha mashindano. Kila la heri katika hatua zinazofuata!





