RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI Dkt : HUSSEIN ALLY MWINYI AMEJUMUIKA NA WAISLAAM KATIKA SWALAATUL JUM'A

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Msikiti Taubat , Michungwa Miwili, Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

 Baada ya Sala ya Ijumaa Rais Dkt, Mwinyi aliwaongoza Waumini katika Sala ya Maiti ya Marehemu Haroub Muhammed Kassim aliefariki jana iliofanyika Msikitini hapo na baadae kuifariji Familia Nyumbani kwa Marehemu na kuwataka kuwa na Subira wakati huu wa Msiba huo Mzito.


Wakati huohuo Rais Dkt, Mwinyi alitoa Mkono wa pole kwa familia mbili zilizofiwa hivi karibuni .

Familia hizo ni ya Marehemu Kanali Masoud Khamis ya Mitiulaya pamoja na Familia ya Marehemu Mzee Haji Machano ya Kikwajuni Majabalini aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.




MY MEDIA DIGITAL

Karibu My Media Digital! Hii ni blog inayohusu ubunifu wa kidigitali, ikihusisha video editing, graphic design, na content creation. Tunakuletea mbinu bora na maarifa ya kusaidia kuboresha kazi zako za digital media. Endelea kufuatilia kwa mafunzo, makala, na updates za kisanaa!

Post a Comment

Previous Post Next Post