SERIKALI KUJENGA STANDI YA KISASA KATIKA HALMASHAURI YA WIRAYA YA RORYA
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali imepanga kujenga standi ya Kisasa katika Halmashauri ya wilaya ya Rorya ili kusaidia upatikana wa huduma za usafiri na kuongeza mapato katika Halmashauri hiyo.
Mhe. Dkt. Dugange ameyasema hayo wakati wa maswali na majibu wakati akijibu swali la Mhe. Jafari wambura Chege (Mb) mbunge wa Jimbo la Rorya aliyetaka kujua “Je, kuna mpango gani wa ujenzi wa stendi Wilayani Rorya ili kuongeza mapato ya Halmashauri.” katika Bunge la bajeti linaloendelea Jijini Dodoma.
”Serikali inatambua umuhimu wa Wananchi wa Rorya kuwa na Stendi ya Mabasi kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi. Kwa sababu hiyo, Serikali kupitia Halmashauri imetenga eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 10 katika Kijiji cha Mika na Nyasoko kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya Wilaya ya Rorya.” Mhe. Dkt. Dugange


