Kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sasa ameripotiwa kufariki dunia akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, baada ya kukamatwa kwa tuhuma za wizi wa simu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu na marafiki wa marehemu, kijana huyo alikamatwa na kupelekwa kituoni ambapo inadaiwa aliteswa vibaya kwa kushinikizwa kuwataja aliowapa simu hiyo. Ili kujiokoa dhidi ya mateso, alimtaja rafiki yake ambaye naye alikamatwa. Hata hivyo, baada ya mahojiano na mateso makali, rafiki huyo alionekana kutokuwa na taarifa zozote na akaambiwa amtaje mtu mwingine – ndipo alipomtaja kaka yake ambaye naye alikamatwa.
Baada ya muda, familia ilielezwa kuwa kijana aliyekuwa mtuhumiwa wa kwanza "amejichoma kisu na mapanga" akiwa ndani ya ofisi ya mpelelezi. Wakati wakielezwa hayo, walihoji vipi kisu na mapanga viliingia ndani ya ofisi ya uchunguzi – majibu waliyopata yalikuwa kwamba "kisu hutumika kulia matunda," huku kuhusu panga hakukuwa na majibu ya moja kwa moja.
Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika Hospitali ya Amana, ambapo familia haijapewa rasmi ili kuupumzisha. Wameambiwa kuwa watakapokuwa tayari kuuzika, ndipo wataukabidhiwa mwili – tayari ukiwa umeandaliwa.
Familia na
wananchi wanataka uchunguzi huru na wa kina kufanyika ili kuhakikisha haki inapatikana na ukweli wa tukio hili lenye maswali mengi kufahamika.
SUBSCRIBE CHANNEL YETU KWA TAARIFA ZAIDI | BILA KUSAHAU KUBOFYA KENGERE YA NOTIS ●💯 👇



